Kurunzi ya Sarufi ya Kiswahili – Shule za Upili

Authors

Erick Ochieng'

Synopsis

Kitabu hiki kimeandikwa kwa ustadi ili kumwezesha mwanafunzi kumudu mtaala mpya unaolenga umilisi wa lugha kwa njia sahihi na yenye mvuto ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi kulingana na maelekezo ya Wizara ya Elimu. Kitabu hiki vile vile kimeshugulikia mada mbalimbali kwa namna ambayo kitamwezesha mwanafunzi kuelewa kikamilifu mada husika. Mada zote zinahusu sarufi kwa shule za upili kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne. Mada hizi zimeshugulikiwa kwa uangalifu na kwa umakinifu ili kumjenga mwanafunzi kwa kumpa nafasi ya umilisi wa lugha ya Kiswahili. Kuna mifano na mazoezi anuawi zitakazomwezesha mwalimu kupima umilisi wa mwanafunzi kutoka katika mada mbali mbali za lugha. Mbinu mbali mbali zimetumika kama vile mifano na kujadili hoja. Mbinu hizi zitamsaidia mwanafunzi kuelewa mada kwa njia rahisi zaidi.

Utafiti Academic Press

Published

2022

Categories